MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA COMPUTER

kutokana na ukuaji wa teknolojia watu wengi wamekuwa wakivutiwa kumiliki computer kwaajili ya matumizi mbalimbali.
kimsingi sokoni ku aina nyingi za computer na zikiwa zinatofautiana kwenye swala la ubora.
lakini pia uchaguzi wa computer hutegemeana na matumizi ya muhusika.
kwenye makala hii nitagusa mambo kadhaa ambayo ninadhani ni muhimu kuyazingatia unapotafuta computer ya kununua.
1. UKUBWA WA HARD DISC.
unapitaka kununua computer iwe kwaajili ya kuhifadhia vitu au kwaajili ya kuitumia kama ofisi yako basi ni muhim kuangalia ukubwa wa hard disc ukilinganisha na bei, hii ni muhim kwasababu udogo wa hard disc huleta matatizo mengine kwa mtumiaji ikiwemo computer kuwa slow, au kuingia gharama ya kununua hard disc mpya au external. kimsingi computer huwa na hard disk za ukubwa tofaut kuanzia 64GB mpaka 2TB.
kwa ushauri wangu ni vema ukapata compuger yenye ukubwa usiopungua 250GB. hapa unaweza kugawa pertition mbili yaan local disc C  ambayo ni operating disc utaipa 100GB na Local Disc D ambayo hii utatunzia vitu vyako utaipa 150GB
2. UKUBWA WA RAM
neno Ram ni kifupi cha neno RANDOM ACCESS MEMORY. kazi kubwa ya Ram ni ku control kila tendo linalofanyika kwenye computer, yaan mfano unapofungua file lolote taarifa ni lazima iende kwenye RAM itunzwe huko kwa muda mfupi ndio file liweze kufunguka.
kwa mantiki hiyo RAM inapokuwa ndogo basi na computer nayo inakuwa slow sana.
sasa hapa kama nilivyosema awali inategemea unataka computer kwaajili ya nini?
kwa mapendekezo yangu napendekeza ununue computer yenye RAM isiyopungua nne kama una matumizi ya kawaida.

3.UKUBWA WA PROCESSOR na AINA YA PROCESSOR.
hiki ni moja ya kitu muhim kwenye computer, hiki tunaweza kukiita ubongo wa computer. maana hapa ndipo taarifa zote za computer zinapotafsiriwa.
udogo wa processor huwez kusababisha matatizo mengi kwenye compuer.
kwa upande wangu napendekeza watu kununua computer kuanzia core I3 kwa matumizi ya kawaida au AMD A5.
pia mimi napendekeza processor za intel kwasababu bado zinaonekana ni bora ukilinganisha na nyingine.

4. TOLEO LA COMPUTER(GENERATION)
Hiki ni moja ya kitu muhimu kukiangalia unapotaka kununua computer. 
watu wengi huwa hatuangalii hii lakini ni ukweli usiopingika kwamba generation mpya huwa zinakuwa vizuri sana ukilinganisha na Generation za zamani.
mfano, unaweza kukuta computer ni CORE i5 lakini genration ni ya 3. hii ubora wake haiwez kulinganishwa na Core i5 hiyo hiyo generation ya 6 au ya 9.
mimi napendekeza ununue computer inayoanzia generation ya 5.

5.UHAI WA BETRI
hii nadhani inajieleza kabisa. kama unanunua laptop maana yake una lengo pia la kuepukana na matatizo ya umeme na kutokusave projects au kazi ulizokuwa unazifanya. kwahyo hapa ni muhim kupata computer ambayo inaweza kukaa na chaji hata saa moja. ila ukiipata inayokaa masaa mengi zaidi ni bora zaid.

6.BAJETI YAKO.
kiukweli computer bora ni gharama, na kila nilichoandika hapo juu kinaweza kufanikiwa kama tu bajeti yako itakuwa nzuri, lakini pia bajeti ya ununuzi wa computer inategemea na matumizi.
zipo computer kuanzia laki mbili na nusu mpaka milion 4.
kwa matumizi ya kawaida napendekeza ununue computer inayoanzia laki 3 na nusu mpaka laki 6.
inategemea na ulivyojipanga, pia inagegemea na hali ya computer yenyewe.

NI MATUMAINI YANGU SOMO HILI LIMEKUPA MWANGA.
imeandaliwa na
OBBY MJUZI
CEO
WATU MAKINI TECHNOLOGIES

Chapisha Maoni

2 Maoni

Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)