Kupitia somo la leo utaenda kujifunza jinsi ya kuongeza space ya hadi GB 35 Kwenye computer yako.
kabla sijaanza somo hili niseme mambo machache.
1. kama unahitaji kujifunza masomo mbalimbali ya computer kwa undan zaidi basi nakushauri jiunge na darasa langu linalopatikana online, kupitia darasa hilo utajifunza masomo mbalimbali kama vile Microsoft Word, Excel, graphics design, jinsi ya kutengeneza blog, jins ya kutengeneza website, jinsi ya kuagiza vitu kutoka china. gharama za masomo haya zinatofautiana kulingana na aina ya somo.
masomo.yote yanatolewa kwa njia ya video hatua kwa hatua, na usipoelewa unaruhusiwa kuuliza chochote.
kama unahitaji nichek kwa email yangu mjuzishule@gmail.com.
twende darasani
unaweza kufanikisha hili kwa kufuata hatua zifuatazo.
1. bonyeza windows button na E kwa pamoja. au nenda kwenye my computer kwa unaetumia windows 7.au this pc kwa unaetumia windows 10.
2. Right click kwenye local disk C (ile disk yenye windows) kisha chagua Properties
3. chagua sehemu wameandika Disk cleanup kisha bonyeza yes kama utaletewa ujumbe wa kukubali
4. weka tick kwenye vibox vyote upande wa kusho mwa ukurasa utakaofunguka
5. bonyeza sehem wameandika delete previous files, au clean system files. (kwa kawaida inakuwaga chini baada ya hizo sehem ulizoweka tick, na inakuwa na ki alama cha tofaut upande wake wa kushoto.
6. bonyeza yes kama itakuomba ruhusa ya kufuta kisha bonyeza ok.
IMEANDIKWA NA
OBBY MJUZI
KUTOKA WATU MAKINI TECHNOLOGIES

0 Maoni