JINSI YA KUFUFUA FLASH ZILIZOKUFA. SEHEMU YA KWANZA

flash zimekuwa zikipata matatizo mbalimbali na kusababisha kutofanya kazi katika ubora unaotakiwa, au kushindwa kufanya kazi kabisa. yapo matatizo mengi ya flash yanayowasumbua watu, na leo nitaanza na tatizo la kwanza. tatizo hili linaitwa WRITE PROTECTION.

kabla sijaanza somo hili niseme mambo machache.
1. kama unahitaji kujifunza masomo mbalimbali ya computer kwa undan zaidi basi nakushauri jiunge na darasa langu linalopatikana online, kupitia darasa hilo utajifunza masomo mbalimbali kama vile Microsoft Word, Excel, graphics design, jinsi ya kutengeneza blog, jinsi ya kutengeneza website, jinsi ya kuagiza vitu kutoka china. gharama za masomo haya zinatofautiana kulingana na aina ya somo.
masomo.yote yanatolewa kwa njia ya video hatua kwa hatua, na usipoelewa unaruhusiwa kuuliza chochote.
kama unahitaji nichek kwa email yangu mjuzishule@gmail.com.
twende darasani

inawezekana wewe ni mmoja kati ya watu waliojaribu kuweka au kutoa  vitu kwenye memory card au flash na ukaletewa ujumbe kwamba the disk is write prottected, na ukaona kabisa hii flash imekufa na haiwez kufanya kazi yoyote

basi habari njema ni kwamba hizi flash zinaweza kutibiwa kwa kutumia njia mbalimbali yaani commands au hata softwares. leo nitakuelezea njia ya command lakin pia kama itashindikana bas kwenye somo la pili nitakuwekea softwares bure za kutatua swala hili.

fuata hatua hizi kwa usahihi.

1. bonyeza windows button na R kwa pamoja kitatokea kitu kama hiki hapa chini then andika CMD kisha bonyeza ENTER

Remove write protection with diskpart command prompt2. kitatokea kipage cheusi kama hiki hapa chini, hiki ndio huitwa COMMAND PROMPT au CMD kama inavyojulikana kwa kifupi. kitu hiki kinaweza kufanya kazi nyingi sana ikiwemo kuondoa virus walioshindikana, tutajifunza siku moja somo hili. aya sasa

 Andika diskpart  kama inavyoonekana hapa chini kisha bonyeza enter.

Remove write protection with diskpart command prompt

3: andika lisk disk kama inavyoonekana hapa chini kisha bonyeza enter 

Remove write protection with diskpart command prompt4. hapa zitatokea disk zote zilizochomekwa kwenye comouter yako ikiwemo na hard disk yako, kuwa makini kuchagua flash unayotaka kuifanyia kazi kwa kuangalia ukubwa wa hiyo flash, andika select disk 2, hapo kwenye "disk 2" wewe utaweka namba ya flash yako, mimi nimeweka 2 kwasababu ndio namba ya flash yangu.

Remove write protection with diskpart command prompt

5. andika  attributes disk clear readonly kisha bonyeza enter

Remove write protection with diskpart command prompt6. hapo utakuwa umemaliza na flash yako itakuwa imepona na kuanza kazi kama kawaida.

kama njia hii haitakusaidia basi usikose kufatilia somo lijalo nitaelekeza njia nyingine 4 za kukusaidia kwenye matatizo yako, kama una swali lolote tafadhali andika comment yako hapo chini.

NAITWA OBBY MJUZI

KUTOKA WATU MAKINI TECHNOLOGIES.

Chapisha Maoni

0 Maoni