JINSI YA KU RESET SIMU ZA SAMSUNG

Wanakwetu salaam.
leo nimeona nikushirikishe somo hili rahisi, ambalo naamin litakuwa msaada mkubwa kwako. watu wengi tumekuwa tunataman ku reset simu zetu kutokana na matatizo mbalimbali iliwemo kusahau password na mengine mengi. kabla sijaanza somo hili niseme mambo machache.
1. kama unahitaji kujifunza masomo mbalimbali ya computer kwa undan zaidi basi nakushauri jiunge na darasa langu linalopatikana online, kupitia darasa hilo utajifunza masomo mbalimbali kama vile Microsoft Word, Excel, graphics design, jinsi ya kutengeneza blog, jins ya kutengeneza website, jinsi ya kuagiza vitu kutoka china. gharama za masomo haya zinatofautiana kulingana na aina ya somo.
masomo.yote yanatolewa kwa njia ya video hatua kwa hatua, na usipoelewa unaruhusiwa kuuliza chochote.
kama unahitaji nichek kwa email yangu mjuzishule@gmail.com
twende darasani kwa kufuata hatua hizi. 
kabla ya kufuata hatua hizi nakukumbusha kwamba hapa tunafuta kila.kitu simu inabaki mpya kama ilivyotoka dukani, kwahyo kama kuna vitu unataka kuhamisha hamisha kabisa.

 1. Zima simu yako

2.bonyeza hom button, batani ya kuongezea sauti na batani ya kuwashia kwa pamoja kwa muda  kisha achia batani ya kuwashia halafu endelea kushikiria hizo mbili mpaka itakapokuja nembo ya android

3. ikija nembo ya android achia batan zote halafu bonyeza batani ya kuongezea sauti 

4. itakuja system recovery.

5. tumia batani ya kupunguzia sauti kushuka mpaka sehem wameandika "wipe data/factory reset

6. utakuja ujumbe unaosema delefe all user data,

7. bonyeza batani ya kuwashia kisha iache ifute kila kitu.

8 ikimaliza kufuta tumia batani ya kuongeza sauti kuchagua reboot system now.

9. iache simu itazima kwa muda na kuwaka tena, utakuwa umemaliza.

***jifunze kila kitu jifunze kila siku***

IMEANDIKWA NA

OBBY MJUZI

KUTOKA WATU MAKINI TECHNOLOGIES


Chapisha Maoni

0 Maoni