SOFTWARE 10 UNAPASWA KUWA NAZO KWENYE COMPUTER YAKO


Na obby mjuzi

Wanakwetu habari, leo nimeona nishare nanyi somo hili dogo, hii ni kutokana na maswali mengi ninayopokea kutoka kwa wanakwetu wanaofatilia masomo yangu.
sasa kabla ya kuanza somo letu la leo niseme mambo machache
Kama unataka kujifunza mambo ya computer kwa undani jiunge na darasa ninalofundisha online, darasa hili linahusisha watu wa aina zote pia watu wa sehemu zote, uwe umesoma IT au hujasoma, masomo yanatolewa kwa njia ya video hatua kwa hatua, muda na gharama hutofautiana kulingana na somo husika. Ndani kuna masomo kama
• Jinsi ya kutengeneza blog
• Graphics design
 • Website development(HTML)
 • Website designing (CSS)
 • JAVA
 • PHP
 • DATABASE
 • Microsoft office
          Microsoft word
          Microsoft excel
          Microsoft power point
         Microsoft publisher
         Microsoft access
Kwa unaehitaji kujiunga nicheki kwa email mjuzishule@gmail.com
Tuendelee……..
hizi ni software 10 unazozihitaji kwenye computer yako.

1.microsoft office.
Hii ni moja ya program muhim sana kwenye Computer yako. Kama tujuavyo software hii inajumuisha microsoft word ambayo hukusaidia kuchapa(kutype) kazi mbalimbali, microsoft excel ambayo hutumika kama database pia huweza kufanya kazi mbalimbali za kihesabu, microsoft powerpoint ambayo ni muhim sana kwenye kufanya presentation, microsoft database kama jina lake linavyojieleza, microsoft publisher hii n kwa wale mnaopenda kuwa waandishi wa vitabu vyenye ubora, pia wengine hutumia kwenye kudesign mambo mbalimbali japo wengi wetu tumehamia kwenye photoshop, na illustrator.
Napendekeza utumie office ya 2007, 2010. au 2019, Maana hazisumbui. ingia kwenye app yangu kuweza kuzipata zote hizo.

2.MEDIA PLAYER
Media player ni software zinazotumika kuplay video au mziki kwenye computer yako, ziko aina nying za media player ikiwemo windows media player, QQ player, VLC na nyingne nying. Hapa watu wengi hufanya makosa kwasababu huweka media player zaid ya moja wakisahau kwamba kuwa na software nying kunafanya computer iwe slow kwahiyo ni vema kuchagua software moja unayoiamini na kuipenda ili uitumie badala ya kuwa na media playe r nyingi bila sababu, mimi napendekeza utumie VLC kwasababu huwa haisumbui na inasaut ambayo ni standard

3.BROWSERS
browser ni software inayokuwezesha kuingia kwenye mtandao(internet) Ipo aina nyingi za browser ikiwemo opera, mozilla, uc browser, google chrome, na nyingne nying. Pia watu wengi hukosea hapa wanaweka browser kama 7 tofauti wakidhani ni fasheni kumbe hawajui kwamba wanasababisha computer kuwa slow. Mimi napendekeza uchague chrome na opera. Hii ni kutokana na ubora na security zinazopatikana kweny browser hizi pia na ubora zilionayo.

4.CONVERTER.
hiizi ni software zinazotumika kuconvert nyimbo kuwa au picha kuwa katika formar mbalimbali, mfano unaweza kubadil video kuwa audio au format flan ya video kuwa format nyingine. Unaweza kudownload video kweny mtandao na unapojaribu kuiplay kwenye deki inakwambia unsurpported format maana yake unahitaj converter ili uweze kubadili video hiyo iwe katka mfumo utakaokubali kucheza kwenye deki, deki nying hutumia VOB au MPEG format.
Napendekeza utumie format factory kutokana na ubora wake.

5.ADOBE READER & ADOBE PLAYER.
hizi ni muhim sana kwenye computer yako kwasababu adobe player ni tofaut na zile media player nyingne nilozotaja hapo juu hii hutumika kuplay video za mtandaoni mfano youtube vdeos au facebook videos. Kwahiyo ni muhim kuwa nayo hii. Adobe reader hutumika kufungua vitabu na documents mbalimbali zilizo katka mfumo wa PDF kwahiyo ni muhim kuwa nayo. Napendekeza utumie adobr 9 au 12. Maana ni rahis zaid kutumia.

6.ANTIVIRUS.
hii ni itakusaidia kuikinga computer yako dhidi ya virus, zipo aina nyingi za anti virus ikiwemo avast, malwarebyte, kaspersky, avg, avira, smadav, Na nyingine nyingi tu.
mimi napendekeza utumie malwarebyte.
Kwasababu uzuri wa hii ukiingia kwenye website ambayo sio salama haifunguki.
Pia inauwezo mkubwa wa kudetect virus.
Niliwah toa somo jinsi ya kuitest anti virus yako kama ni active au la, ingia kwenye app yangu utalikuta.
Kumbuka kuwa na anti virus zaid ya moja ni virus tayari. Hivyo usitumie ant virus zaid ya moja.

7.WINRAR.
watu wengi hawajui umuhim wa hii software, na pengine hawaijui kabisa.
Winrar ni moja ya software muhm kwenye computer yako kwasababu inaweza kutumika kulock ma folder, pia inaweza kutumika kuzip mafolder au ku un zip mafolder.
Hii ni free software hivyo ingia google na udownload na uinstall.

8.DOWNLOAD SOFTWARE.
Zipo program nying zinazotumika kudownload vitu mbalimbali kwenye mtandao. Wengine hutumia internet download manager, youtube downloader, na downlkaders nyingne nyingi.
Kwa mtu usie na uelewa sana na mambo ya computer ni muhim kuwa na downloader ila kwa mtu ulie na uelewa uelewa sio muhim sana kuwa na downloader maana kuwa na software nying kwenye sim yako inaweza kusababisha pc iwe slow.
Mimi napendekeza utumie internet download manager kwasababu ipo faster sana, pia uzuri wake ni kwamba unapoishia inaweza kuendelea.
Pia napendekeza utorents kwa zile web zinazohitaj utorents maana nayo ni nzuri sana.
In case idm yako inakwambia faje serial, ingia kwenye blog yang kuna somo linaloelezea haya na jinsi ya kutatua(kwa njia ya vdeo)

9.PICASSA
hii ni software inayotumika kufungua picha kwenye computer yako. Zipo aina nyingi za hizi software, ila nimependekeza hii kwasababu ni bora pia inaweza kutumika kama photo editor.
Ni free software ingia google utaipata

10.DICTIONARY.
nadhan wengi tunaelewa maana ya hii. Nimependekeza kama ya kumi na ya mwisho kwasababu ni muhm kujielimisha hivyo dictionary ni muhim.
NOTE
hizi ni software muhim kuwa nazo.
Ila simaanishi uwe nazo hizi tu. Idadi ya software unazotakiwa kuwa nazo zinategemea ukubwa wa RAM yako na PROCESSOR.
kama hivyo ni vikubwa basi unaweza kuweka software nying zaidi.
Ila kama ni ndogo usiweke kwasababu computer itakuwa slow.
>>>MWISHO<<<
*Imeandaliwa na*
*OBBY MJUZI©2016*
mjuzishule@gmail.com
0753217400
*WATU MAKINI*

Chapisha Maoni

2 Maoni

Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)