JINSI YA KUJUA UHAI WA BETRI YA COMPUTER YAKO

mwanakwetu salaam, leo nimeona nikushirikishe somo hili rahisi nikiamini linaweza kuwa msaada mkubwa kwako.
watu wengi tunapenda kutumia computer ikiwa na betri isiyosumbua, ila wengi wetu hatujui uhai wa computer zetu.
kupitia hatua hizi chache utajifunza namna nzuri ya kutambua uhai wa betri ya computer yako. 
1.nenda sehem ya kusearch andika
cmd
2. kitatokea kidude cheusi hicho ndicho kinaitwa cmd(command prompt)  right click halafu chagua "run as administrator"
3. kikifunguka andika hii command powercfg  /batteryreport  halafu bonyeza enter
4. hapo tualetewa directory kama unavyoiona hapa chini. sasa chakufanya copy hiyo directory kama unavyoona hapa chini
5. fungua browser yako yoyote, (browser inaweza kuwa opera, chrome, mozila, ucbrowser na nyingine nyingi)
6. paste ile directory yako halafu bonyeza enter.
7. hapo utaletewa repoti nzima ya betri yako na uhai wake.

IMEANDALIWA NA
OBBY MJUZI
CEO
WATU MAKINI TECHNOLOGIES

Chapisha Maoni

0 Maoni