katika somo la leo tutakwenda kujifunza jinsi ya kuficha au ku hide folder lako bila kutumia software yoyote. hili ni moja kati ya maswali niliyoulizwa na wafuatiliaji wa APP yetu.
pia kama wewe una swali lolote na ungependa tulizungumzie basi nitumie kwa email yangu mjuzishule@gmail.com.
pia kama unahitaji kujifunza graphics design, jinsi ya kutengeneza blog, jinsi ya kutengeneza website, na masomo.mengine bas jiunge na online class kwa gharama nafuu.
masomo yanafundishwa kwa njia ya video hatua kwa hatua.
TUENDELEE....
kabla hauja hide folder kwanza unatakiwa kuwa na kitu kinaitwa folder directory,
hii tunaipata kwa kufata hatua hizi mbili
a) fungua folder unalotaka kuli hide
b) sehem ya juu utaona maneno yaliyo katika mfumo huu
mfano C:/desktop/obby
angalia hii picha hapa chini
c) copy hayo maandishi kama halivyo, kisha fata hatua hizi chini
1.bonyeza Windows button na R kwa pamoja.
2. andika CMD kisha bonyeza ENTER
3. andika command hizi attrib +s +h weka directory ya hilo folder uliyoicopy pale juu.
mfano attrib +s +h c:/desktop/obby
4. bonyeza ENTER na folder litapotea.
JINSI YA KULIRUDISHA
fata hatua hizo zote ila kwenye hatua namba 3 badilisha weka alawa ya - badala ya +.
yaani isomeke
attrib -s -h halafu weka directory ya folder
IMEANDALIWA NA
OBBY MJUZI
CEO
WATU MAKINI TECHNOLOGIES
0 Maoni